Sunday, May 8, 2016

Wananchi Waombwa Kutaja Wanaouza Sukari Bei ya Juu...Wanaouza Zaidi ya Bei Elekezi ya 1800 Kuchukuliwa Hatua za Kisheria na Kunyang’anywa Leseni


Ofisa Biashara Wilaya ya Bukombe, Celestin Mwamba amewataka wananchi kuisaidia Serikali pindi watakapobaini ukiukwaji wa agizo la uuzwaji wa sukari zaidi ya bei elekezi ya Sh1, 800 kwa kilo.

Mwamba alisema kila mwananchi awe mdadisi kwa kuwa mfanyabiashara anatakiwa kuuza sukari kwa bei halali iliyoelekezwa na Serikali ambayo ni sawa na Sh90,000 kwa gunia lenye ujazo wa kilo 50.
Alisema hayuko tayari kufumbia macho wafanyabiashara wanaouza kilo ya sukari kwa Sh2,400 na atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria na kunyang’anywa leseni.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, James Ihunyo alisema wafanyabiashara hawaruhusiwi kuficha bidhaa hiyo kwenye stoo zao kwani kufanya ni ukiukwaji wa agizo la Serikali na atakayebainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Ihunyo aliwataka wananchi kuwafichua wanaouza bidhaa hiyo kwa kufika oisini kwake ili wadhibitiwe mapema.
Mfanyabiashara wa rejareja wa sukari mjini Ushirombo, Jackline Petro alisema wanalazimika kuuza kwa bei ya juu kutokana na jinsi wanavyouziwa katika maduka ya jumla.

Credit: Mwananchi
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger