Mtoto wa umri wa miezi saba, aliyeokolewa baada ya kukaa kwenye vifusi kwa siku nne, ametambuliwa na kukutanishwa na baba yake.
Baba yake mtoto huyo, Bw Ralson Wasike, akihutubia wanahabari, amesema bintiye amekuwa na nguvu sana.Amesema alikuwa na wasiwasi sana baada ya kumtafuta siku hizo zote na kumkosa.
Mtoto
huyo alitolewa kwenye vifusi kwenye saa kumi usiku na kupelekwa
hospitalini kwa mujibu wa maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu.
Alipatikana akiwa amefunikwa kwa blanketi ndani ya ndoo na hakuonekana akiwa na majeraha yoyote.Bw Wasike amesema alijawa na furaha sana baada ya kusikia kwamba
mtoto huyo alikuwa hospitalini, lakini anasema bado hajafanikiwa kumpata
mkewe.
Mtoto huyo ni miongoni mwa manusura waliookolewa baada ya
jumba la ghorofa sita kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi baada ya
mvua kubwa kunyesha Ijumaa.
Mwingine aliyeokolewa ni mtoto wa
umri wa mwezi mmoja, kwa jina la Joy, aliyetolewa kwenye vifusi saa nane
baada ya jumba hilo kuporomoka.
Mama yake Mildred aliambia BBC kwamba alikuwa na furaha sana kumpata tena mwanawe.Juhudi za uokoaji bado zinaendelea na watu 95 bado hawajulikani walipo.Watu 22 wamethibitishwa kufariki.
Wale waliokuwa wakiishi katika jumba lililoporomoka wamejengewa makao ya muda ambapo wanahudumiwa.
Wahisani wanawasaidia kwa chakula na mavazi.
0 comments:
Post a Comment