Katika siku mbili za kujadili bajeti ya wizara ya maliasili na utalii iliyoomba kutengewa kiasi cha Sh. 135,797,787,000 katika hotuba iliyowasilishwa na Waziri wake Jumanne Maghembe, Wabunge walipata nafasi pia ya kuchangia ambapo hapa nakukutanisha na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega
Wakati
mwingine hata mimi nashawishika kufikiria kwamba kabla hatujaingia
kwenye jengo hili tuwe tunapimwa kama tumevuta marijuana, katika hali ya
kawaida kijana hata kama umepigiwa kura na kuaminiwa na wananchi
ukaenda kutukana lazima utakuwa na tatizo kwenye akili yako‘
‘Jana
yupo mwenzetu mmoja wa kutoka chama ninachotoka amezungumza mambo ya
ajabu sana hapa, unaweza kuona ni kwanamna gani watu hawaelewi ni nani
katika nyumba hii ameingia bila ya Chama kilichomleta, wote tumezaliwa
na vyama vyetu’
‘Watu
wa Dar es salaam bado wanatumia nishati ya mkaa, na Serikali inapiga
vita matumizi ya mkaa. Nimwambie Waziri nguvu tunayotumia kupiga vita
matumizi ya nishati hii, tutumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha
tunawatafutia nishati mbadala Wananchi hawa‘
‘Tunawaambia
watumie gesi hata elimu yenyewe ya matumizi ya gesi inafahamika?
matumizi ya gesi hayakuanza leo, hata wasomi wenyewe wanaogopa kutumia
gesi. Sasa tufanye jitihada za kutoa elimu kabla ya kuwaambia wasitumie
wasitumie..!‘
Endelea kumsikiliza Mbunge Abdallah Ulega hapa chini kwenye hii Video…
0 comments:
Post a Comment