Saturday, April 6, 2013

VIFO VYA KIFUSI ARUSHA, WATU WADAI NI KAFARA

VIFO vya watu 14 waliofariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha moramu mkoani hapa vimedaiwa kuhusishwa na kafara ya wafanyabiashara maarufu.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake, wafanyabiashara wengi mkoani humo wamekuwa wakiamini kuwa ili biashara zao zifanikiwe lazima watoa kafara ya kuua watu.


“Siyo bure ile ni kafara na mambo ya kishirikina, haiwezekani watu wafunikwe udongo kwa pamoja pasipo kuwa na dalili zozote za kuanguka kwa kifusi hicho.
“Freemason pia wameingia sana Arusha na wamewateka watu wengi,  hivyo matukio kama haya lazima yatokee haswa vifo vya vijana wadogo ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa,” kilisema chanzo hicho.
Aprili 3, mwaka huu ibada ya mazishi ya waathirika wa maporomoko hayo ilifanyika katika Kanisa la Kilutheri, Moshono na ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger