Polisi Mkoa wa Morogoro imekusanya zaidi ya Sh200 milioni kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani katika kipindi cha kuanzia Aprili Mosi hadi Aprili 30 mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (pichani) alisema jana kuwa ukusanyaji wa fedha hizo umetokana na operesheni maalumu iliyofanywa na jeshi hilo.
Matei alisema makosa 7,838 yaliyobainika kutoka katika magari na pikipiki, yalitozwa faini.
Aliyataja makosa kwa upande wa magari kuwa ni mwendo kasi makosa 1,801, ubovu wa magari 909, kukiuka ratiba 230, kuzidisha abiria 117, kutokuwa na bima 111 na makosa mengineyo 2,110.
Pia, alitaja makosa ya pikipiki kuwa ni kutokuwa na kofia ngumu ni makosa 1,189, bima 248, kuendesha bila leseni 168 na mengine 955.
Kamanda Matei aliwataka waendesha pikipiki na magari kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani kama zinavyoelekeza, huku akiwasihi watumiaji hao kuacha kutoa ukaidi kwa askari wa usalama barabara pindi wanaposimamishwa kufanya ukaguzi katika magari.
Katika tukio jingine, mkazi wa Kijiji cha Nyae, wilayani Kilombero anatafutwa kwa tuhuma za kufanya ubakaji kwa mwanafunzi wa miaka 14 wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Muungano.
Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo Mei 4, saa nane mchana wakati mwanafunzi huyo akiwa amelala chumbani kwa dada yake
0 comments:
Post a Comment