Ni Mtoto kutoka Afghanistan Murtaza Ahmadi ambaye
anamkubali sana staa wa soka Lionel Messi na aliamua kuvaa mfuko wa
plastiki wenye mfanano na jezi ya Messi kwenye timu ya taifa Argentina
ambapo Messi alipoiona ile picha alimtumia jezi mbili kama zawadi na
kuziweka saini zake.
Stori mpya ni kuwa baba wa mtoto huyu mwenye umri wa miaka mitano amaeamua kuhamia Pakistan
na familia yake kutokana na kuhofia maisha ya mtoto wake anayeweza
kutekwa au chochote kingine kikatokea sababu baada ya kupewa jezi na
Messi wamekua wakipokea vitisho mbalimbali.
Baba wa
mtoto huyu amesema siku kadhaa zilizopita alipokea simu nyingi kutoka
kwa Wababe waliyedhani Messi katoa hela kwa Murtaza hivyo wanataka mgao
wao, hiyo ni moja ya sababu zilizofanya wahame Afghanistan na kwenda
kuishi Pakistan ambako Murtaza na wenzake saba wa familia hiyo wanaishi
chumba kimoja.
0 comments:
Post a Comment