Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeonya vitendo vinavyofanywa na
baadhi ya watu kuchapisha picha za utupu ama za kutisha katika mitandao
ya kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam , Mkurungenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Helen Kijo Bisimba
alisema kuwa, kumekuwa na matukio kadha yanayofanywa na watu juu ya
kurekodi na kupiga picha ambazo sio nzuri kwa mujibu wa sheria.
Alibainisha
picha hizo kuwa ni pamoja na matukio ya mauaji, ajali za kutisha na
miili ya marehemu zinazochapichwa katika mutandao ya kijamii, blog na
hata baadhi ya vyombo vya habari bila kijali kwamba, kufanya hivyo ni
kinyume cha sheria.
Dk.
Kijo alisema kuwa, tarehe 4 Mei mwaka huu katika Mkoa wa Pwani, Wilaya
ya Bagamoyo picha za miili ya marehemu (mama na mtoto) ambayo majina yao
yamehifaziwa, zilisambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha
majeraha ya kutisha kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa.
Katika
tukio la pili alibainisha kuwa, ilitokea Mkoa wa Kilimanjaro mwaka huu
ambapo picha za maiti ya mtoto aliyeuawa na mama wa kambo zilionesha
akiwa ndani ya jeneza.
Katika
maeneo ya Kibamba Jijini Dar es Salaam, Januari mwaka huu picha za
utupu za mwanamke aliyesemekana kuwa ni msukule aliyekutwa kwenya kisima
zilizambazwa katika mitandao ya kijamii.
Alisema kuwa, hayo ni baadhi ya matukio hivyo jamii inapaswa kutambua kuwa vitendo hivyo ni udhalilishaji na kinyume cha sheria.
“Kwani
kwa mujibu wa haki ya kikatiba ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya 1977 kila mtu ana haki ya kikatiba ya kuthamini
utu wake kuwa faragha akiwa hai au amefariki,” alisema.
0 comments:
Post a Comment