BAADA ya kukiri katika
gazeti hili kuwa ameamua kuokoka na kumrudia Mungu, mrembo kunako filamu
za Kibongo, Kajala Masanja amekejeliwa na baadhi ya watu wake wa
karibu.
Akizungumza na Amani Kajala alisema
kitendo cha kuokoka kimegeuka kama kejeli kwa marafiki zake ambapo wengi
humcheka lakini anaamini kabisa siyo akili zao bali shetani anataka
kuwatumia ili aanguke.
“Kuna ambao wananicheka kicheko kikubwa
kabisa baada ya kusikia kuwa nimeamua kumfuata Yesu na wengine
kunikejeli lakini mimi sina neno naamini kabisa ni nguvu ya shetani ili
nirudi nilikotoka, nawaambia tu watakuwa wamechelewa sana,” alisema
Kajala.
0 comments:
Post a Comment