Janet Jackson ni mjamzito, akiwa na umri wa miaka 49. Atakuwa mtoto wao wa kwanza na mumewe, Wissam Al Mana.
Habari hiyo imekuja baada ya muimbaji huyo kutangaza kusitisha ziara
yake ya Unbreakable kwa kile alichoeleza kama kupanga familia yao.Alisema kuwa alilazimika kufanya hivyo kutokana na maagizo ya daktari.
Chanzo kimoja kiliiambia E! News Jumatano hii kuwa ujauzito wake upo
kwenye trimester ya pili na kwamba yeye na mume wake Al Mana wamekuwa
wakifanya kazi na mtaalam wa masuala ya ushikaji mimba kwa muda.
Ni nadra sana kwa mwanamke wa umri wake kupata ujauzito kwa njia ya
kawaida. Wengi wanaoshika hutumia njia ya IVF, kwa kutumia mayai yao
wenyewe waliyoyagandisha wakati wa miaka yao waliyokuwa na uwezo wa
kuzaa au kupewa yai la wanawake wadogo.
Janet na Al Mana, bilionea wa Qatar mwenye miaka 41 walifunga ndoa mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment