Msanii Snura Mushi ambaye wimbo wake
wa Chura ulipigwa marufuku na serikali ya Tanzania ameomba radhi na
kuahidi kutekeleza maagizo ya serikali.
Wimbo huo ulipigwa
marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ilisema“maudhui ya utengenezwaji wa video ya wimbo huo haiendani na maadili ya
Mtanzania.”
Mamlaka hiyo ilisema kazi hiyo inadhalilisha tasnia ya muziki.Serikali ilipiga marufuku maonyesho yote ya hadhara ya Snura hadi pale
atakapokamilisha usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la Sanaa la
Taifa (Basata).
Akizungumza na wanahabari akiwa ameandamana na meneja wake, Snura
amesema amechukua hatua na kusajiliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za
kisanii
0 comments:
Post a Comment