Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza rasmi kutoitambua
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inayoongozwa na Dk Ali Mohamed
Shein.
Mbali na kutoitambua Serikali hiyo, chama hicho kimesema leo
kitatoa mkakati mzito wa namna ya kushughulikia suala la matangazo ya
Bunge la Kumi na Moja kutoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni.
Msimamo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari jana mjini Dodoma katika
kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji,
manaibu wake wawili, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).
Pia
walitoa taarifa juu ya mambo yanayojadiliwa katika kikao cha siku
mbili cha Kamati Kuu (CC) kinachofanyika chini ya Mwenyekiti wake,
Freeman Mbowe.
Akizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar, Mwalimu alisema
chama hicho hakitampa ushirikiano Dk Shein.
“Kikao maalumu cha Kamati
Kuu ya Chadema kilichoketi Jumatatu, tumefikia msimamo wa kutoitambua
Serikali ya SMZ. Msimamo wa Maalim Seif Shariff Hamad ndiyo msimamo
wetu,” alisema.
Maalim Seif aliwania urais Zanzibar kupitia CUF katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kabla ya Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC), kufuta matokeo yake na kutangaza uchaguzi wa marudio
ambao mgombea huyo na chama chake walisusia.
“Hatutatoa
ushirikiano kwa
SMZ na katika kikao cha leo (jana) cha CC tutawasilisha azimio hilo.Hali
ya kisiasa Zanzibar ni mbaya mbaya sana. Wazanzibari wanaelekea
kununa,” alisema Mwalimu.
Mwalimu alisema hawatafanya maandamano
Zanzibar lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwani Wazanzibari wengi
wanaelekea kununa na kwamba hilo litasababisha hali mbaya zaidi.
“Hali ya
Zanzibar si nzuri kama CCM wanavyoeleza. Watu hawazikani,
hawatembeleani tumerudi kulekule kama mwaka 1995 kabla ya kuundwa kwa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema.
Mashinji alisema kikao hicho cha
kamati kuu kitapokea taarifa kutoka kwa wabunge wa Chadema, kuhusu
Bunge kutoonyeshwa ‘live’ na athari zake kwa wananchi.
“Uhuru wa
wananchi kupata habari litajadiliwa kwa kina. Sasa hivi Bunge letu
liko gizani tunapata habari za kupapasa tu. Tutatoka na mkakati kabambe
wa kushughulikia suala hili,” alisema.
Akizungumza hatua hiyo iliyochukuliwa na Bunge, Mnyika alisema kinachoonekana sasa ni kama chombo
hicho kimetekwa na Serikali na hilo litatolewa tamko zito rasmi leo na
Mbowe mwenyewe.
“Kuna mambo makubwa tuki- yawekea mkakati huwa Serikali
inasalimu amri. Tunataka kutoka kwenye huu mkwamo ili Bunge lionyeshwe
live,”alisema.
Januari 27, Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Nape Nnauye alitangaza Serikali kusitisha matangazo hayo ya moja kwa
moja kama njia ya kubana matumizi.
Waziri huyo aliliambia Bunge
matangazo hayo yatarushwa vipande muhimu vya mijadala usiku katika
kipindi maalumu cha Leo katika Bunge ambacho kitarushwa saa nne za usiku
uamuzi ambao ulipingwa vikali ndani na nje ya Bunge.
Leo, Nape
atawasilisha bajeti ya wizara yake bungeni ambako mjadala mzito
unaotarajiwa kulitikisa Bunge ni suala hilo la kutoonyeshwa moja kwa
moja kwenye televisheni.
Wadau wa habari wamepiga kambi mjini hapa
kujaribu kuishawishi Serikali na Bunge kubadili msimamo huo
0 comments:
Post a Comment