ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
Ludovick Utouh, amefichua siri ya Rais Dk. John Magufuli kutumbua majipu
kwa kasi, tangu ameingia madarakani mwaka jana.
Akizungumza wakati wa kuzindua ripoti mbili za Mpango wa Uhamasishaji
Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (TEITI), mjini Dar es
Salaam jana, Utouh alisema akiwa CAG aliandaa ripoti nyingi ambazo
utawala uliopita haukizifanyia kazi.
Alisema Rais Magufuli anatumia ripoti hizo kutumbua vigogo mbalimbali, kwa sababu amekuta mambo yako mezani.
“Ripoti zangu nikiwa CAG ndizo zinasomwa bungeni, zimeonyesha udhaifu maeneo mbalimbali ya taasisi za Serikali na nyingine.
“Ripoti zangu nikiwa CAG ndizo zinasomwa bungeni, zimeonyesha udhaifu maeneo mbalimbali ya taasisi za Serikali na nyingine.
“Nyingi zilikabidhiwa zamani,viongozi waliopita hawakuzifanyia
kazi…nawaambua utumbuaji majipu unaofanywa na Rais Magufuli, utasaidia
kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato na nidhamu sehemu za kazi.
Alisema ni jukumu la kila mwananchi kulinda rasilimali zilizopo na kwa kufanya hivyo, mapato yataongezeka.
Kuhusu sheria ya madini iliyopitishwa mwaka jana, inayozungumzia uwazi na uwajibikaji katika sekta ya madini, Utouh alisema imesaidia kuleta nidhamu katika sekta hiyo, kwa sababu kabla ya hapo mapato mengi yalikuwa yakipotea.
Kuhusu sheria ya madini iliyopitishwa mwaka jana, inayozungumzia uwazi na uwajibikaji katika sekta ya madini, Utouh alisema imesaidia kuleta nidhamu katika sekta hiyo, kwa sababu kabla ya hapo mapato mengi yalikuwa yakipotea.
Naye Mwenyekiti wa TEITI, Jaji Mark Bomani alisema taarifa za kazi za
TEITI katika ripoti ya mwaka 2013/14, zimesaidia kunufaisha
uhamasishaji uwazi katika sekta ya madini nchini.
Alisema sekta hiyo ilianza kushamiri mwaka 1990, haikuwa na manufaa
kwa uchumi wa nchi kwa vile mapato kwa Serikali hayakuwa wazi.
Alisema mwaka 2007, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete aliunda kamati ya
kuchunguza sekta ya madini ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ikilalamikiwa
na wadau wengi.
Alisema upotevu wa fedha za Serikali mwaka 2009, zilikuwa
hazionekani, lakini CAG Utouh alifanya ukaguzi ambao umesaidia fedha za
madini kuongezeka.
“Ripoti ya mwaka 2014 inaonyesha pato katika sekta hii, limeongezeka
kwa asilimia 10…takwimu zetu zinaonyesha awali kampuni za madini
zilikuwa 11, sasa zimefika 60 zikiwamo kubwa na za kati,”alisema.
Utouh alistaafu rasmi kazi Septemba 2014, baada ya kuitumikia nafasi
hiyo kwa miaka saba alipoteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka
2006.
0 comments:
Post a Comment