Wakati Rais John Magufuli akipambana dhidi ya ufisadi,
uzembe na ukwepaji kodi na uovu mwingine dhidi ya mali za umma, ripoti
mpya ya ukaguzi iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali inaonyesha ana kazi kubwa zaidi kupata ushindi kwenye vita
hiyo.
Ripoti
hiyo ya mwaka 2014/ 2015 iliyowasilishwa bungeni jana na CAG Mussa Juma
Assad imeibua uozo zaidi kwenye halmashauri, taasisi za Serikali na
mashirika ya umma, ikibainisha kuwa nchi ina tatizo kubwa zaidi ya watu
ambao wamekuwa wakishughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Ripoti
hiyo ya pili ya Professa Assad tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo mwaka
juzi, imegusa taasisi zilizowahi kuwa chini ya Rais John Magufuli na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi
Asha Rose Migiro, ambaye alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba.
Ripoti
hiyo pia inaonyesha ufisadi katika ununuzi na uingiaji mikataba
uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), matumizi yasiyo ya lazima
kwenye Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Jeshi la Wananchi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi na
mkoa wa Tabora.
Pia ripoti hiyo imebainisha kuwa mapendekezo mengi ambayo CAG amekuwa akiyatoa kwa takribani miaka saba sasa, hayatekelezwi.
Katika
ripoti hiyo, CAG anaonyesha dosari kwenye utendaji wa Wakala wa Huduma
za Ufundi na Umeme (Temesa), na Wakala wa Barabara (Tanroads), taasisi
zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi ambayo wakati huo ilikuwa ikioongozwa
na Dk Magufuli.
Profesa
Ndalichako alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania
(Necta), wakati NEC imeguswa na ripoti hiyo katika suala la mchakato wa
kuandika Katiba upya ulioongozwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Ripoti
hiyo ya Profesa Assad pia imebainisha kuwa Deni la Taifa, ambalo
hutokana na fedha zinazopowa kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya
kugharimia matumizi ya Serikali, limekuwa kwa tofauti ya Sh7 trilioni.
Tangu
aingie madarakani Novemba 5 mwaka jana, Dk Magufuli amekuwa akitumia
ripoti zilizopita za CAG kusimamisha kazi au kutengua uteuzi wa
watumishi wa umma wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi, lakini amekuwa
akikosolewa kuwa hajaweka mfumo wa kukabiliana na hali hiyo.
Katika
ripoti hiyo, CAG anasema Temesa ilinunua kivuko chenye kasi ndogo
kuliko ilivyotarajiwa na hadi ulipokuwa unafanyika ukaguzi Agosti 2015,
chombo hicho kilikuwa hakifanyi kazi kwa zaidi ya mwaka.
“Kuhusu
dosari katika ununuzi wa kivuko chenye thamani ya Sh7,916,955,000,
Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Umeme, mitambo na ufundi (Temesa)
iliingia mkatabana M/s Johs.Gram-Hanssen Bergensgade 10, DK 2100
Copenhagen Oe Denmark wa ununuzi wa kivuko cha Dar es Salaam –Bagamoyo
chenye thamani ya Dola za Marekani 4,980,000 bila Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT),”anasema CAG.
“Dosari
zifuatazo zilibainika katika manunuzi hayo. Kasi ya kivuko
haikuzingatia matakwa ya mnunuzi. Ripoti ya mtaalamu wa ukaguzi
ilibainisha kwamba kiwango cha juu na chini cha kasi ya kivuko wakati wa
majaribio kilikuwa na kiwango kati ya knots 19.45 na knots 17.25
kinyume na makubaliano yaliyoainishwa kwenye mkataba wa kasi ya kiwango
cha 20,” anafafanua.
“Pili
kivuko kilikabidhiwa bila hati ya makabidhiano Novemba 17, 2014 baada
ya ucheleweshwaji wa siku 16; Pia nilibaini kwamba mpaka wakati wa
ukaguzi, Agosti 2015, hati ya makabidhiano ilikuwa haijatolewa na
mzabuni.”
Ununuzi
wa feri hiyo uliwahi kuzua sakata bungeni huku wabunge wa upinzani
wakilalamika kwamba kilikuwa bomu kwani kinatumia zaidi ya saa tatu kati
ya Dar es Salaam na Bagamoyo badala ya dakika 45 za gari.
Eneo
jingine lililoguswa na CAG ni la malipo yaliyofanywa na Tanroads kwa
makandarasi waliomaliza kazi zao. Kwamba moja ya matatizo makubwa ya
taasisi hiyo ni udhaifu katika menejimenti.
“Wakala wa Barabara (Tanroads) iliingia mikataba mbalimbali ya ujenzi wa barabara na madaraja.
"Wakati
wa ukaguzi nilibaini kwamba baadhi ya mikataba haikukamilika kwa muda
uliopangwa kutokana na kuchelewa kwa ulipaji wa fedha.
"Pia,
nilibaini kwamba ucheleweshwajiwa malipo ya kati ya mikataba 16
ulisababisha ulipaji wa riba kiasi cha Sh 5,616,652,022 na Dola za
Marekani 686,174.86,” alisisitiza CAG.
Profesa
Assad amezungumzia pia ukaguzi maalumu alioufanya kuhakiki fedha
zilizowahi kutolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa taasisi
mbalimbali zilizoko chini yake.
Ukaguzi
huo ulifanywa kutokana na ombi lililowasilishwa na katibu wa Bunge kwa
barua yenye Kumb. NaCBC.155/188/01/26 ya Desemba 19, 2013.
Bunge lilitaka kujua kama fedha zilizotolewa na wizara hiyo kwenda idara na taasisi zilizo chini yake zilipokewa na kutumiwa na wahusika kama ilivyopangwa.
Bunge lilitaka kujua kama fedha zilizotolewa na wizara hiyo kwenda idara na taasisi zilizo chini yake zilipokewa na kutumiwa na wahusika kama ilivyopangwa.
Katika
ukaguzi huo, CAG alibaini kasoro katika vitabu vya akaunti za fedha vya
Necta mwaka 2010, Sekretarieti ya Elimu ya Jumuiya ya Madola, Chuo
Kikuu Huria (OUT), na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Adem).
“Udanganyifu
wa malipo ya Sh185,350,000 yaliyolipwa Necta. Aprili 2010 kiasi cha
185,350,000 kilitumwa Necta kama matumizi ya kawaida. Wakati wa ukaguzi
ilibainika kuwa kiasi hiki cha fedha hakikuandikwa kwenye vitabu vya
uhasibu vya Necta. Hata hivyo, ilibainika kuwa stakabadhi ya mapokezi ya
fedha hizo iliyotolewa na watumishi wasio waaminifu wa Necta ilikuwa ya
kugushi,” anasema.
“Kuhusu
fedha zilizopelekwa OUT ni kwamba kati ya mwaka 2009/2010 Wizara
ilihamisha Sh90,000,000 kwenda Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, ni
kiasi cha Sh40,734,000 ambacho kilipokewa huku Sh49,266,000
hakijulikani.
“Pia
katika mwaka wa fedha 2010/2011 Wizara ilipeleka OUT Sh10,486,252,913
lakini ni Sh10,427,109,020 tu zinazoonekana kwenye vitabu huku
Sh59,143,893 zikiwa hazimo kwenye vitabu.”
Vilevile, CAG amesema katika ukaguzi huo Sh188, 838,528 zilizopelekwa Adem mwaka 2009/2010 zimeyeyuka. Mwaka huo Wizara ilipeleka Sh712,798,788 kwa taasisi hiyo, lakini vitabu vinaonyesha Sh523,960,260 zilipokewa na kurekodiwa, huku Sh188, 838,528 zikikosekana kwenye vitabu.
Vilevile, CAG amesema katika ukaguzi huo Sh188, 838,528 zilizopelekwa Adem mwaka 2009/2010 zimeyeyuka. Mwaka huo Wizara ilipeleka Sh712,798,788 kwa taasisi hiyo, lakini vitabu vinaonyesha Sh523,960,260 zilipokewa na kurekodiwa, huku Sh188, 838,528 zikikosekana kwenye vitabu.
Mbali
ya CAG kuonyesha madudu katika matumizi ya fedha, pia ameonyesha
matumizi mabaya ya Sh7,080 milioni katika mchakato wa uchapaji Katiba
Inayopendekezwa.
“Katika
ukaguzi wangu nilibaini kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ilipokea fedha
kiasi cha Sh7,125 milioni kwa ajili ya kulipia gharama za kuchapisha
vitabu vya Katiba Inayopendekezwa.
"Kutokana
na ufinyu wa muda, Wizara iliomba na kupewa kibali na Wakala wa Huduma
za Manunuzi Serikalini kufanya manunuzi kwa njia ya dharura kupitia
barua yenye kumbukumbu Na CAD.124/318/01/25 ya Desemba 11, 2014,” anasema CAG.
“Katika
ukaguzi wangu nilibaini vitabu vya katiba vilipokelewa kabla ya kuingia
mkataba. Nilibaini kuwa mkataba ulisainiwa Februari 2, 2015, lakini
vitabu vya katiba vilipokelewa Januari 26, 2015.”
Ukaguzi uliofanywa Oktoba Mosi, 2015 umebaini kuwa nakala 158,003 za Katiba Inayopendekezwa zenye thamani ya Sh559,330,620 bado viko stoo au havijatumwa kwa wananchi ili vitumike kwa uhamasishaji.
Ukaguzi uliofanywa Oktoba Mosi, 2015 umebaini kuwa nakala 158,003 za Katiba Inayopendekezwa zenye thamani ya Sh559,330,620 bado viko stoo au havijatumwa kwa wananchi ili vitumike kwa uhamasishaji.
“Kwa
hiyo, haikuwa rahisi kujua kama thamani halisi ya fedha ilipatikana na
lini vitabu hivi vitasambazwa kwa walengwa. Pia, ilibainika kuwa vitabu
hivyo havikujumuishwa kwenye Taarifa za Fedha za Mwaka husika,” anasema.
Katika
ripoti hiyo ya mwaka 2015/16, CAG Assad anasema ukaguzi wake umebaini
matumizi ya mabilioni ya fedha katika ununuzi wa vitu visivyokuwa vya
lazima au bila kuonyesha ushahidi wa malipo husika.
Alibainisha
matumizi ya zaidi ya Sh53 bilioni zilizotumiwa na taasisi sita pamoja
na Sekretarieti mbili za mikoa katika mambo ambayo hayakuwa ya lazima,
kama faini za kuchelewa kulipa kodi ya pango.
Taasisi
hizo ni Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Makazi na Mkoa wa Tabora.
CAG
Assad amebainisha matumizi ya ziada ya Sh109,722, 539 kwa ajili ya
ununuzi wa gari aina ya Toyota Land Cruiser VX V8 kwa Sh297.5 milioni
kutoka kampuni ya Toyota (T) badala ya kutumia mfumo wa ununuzi wa
pamoja ambao ungefanya gari hilo lipatikane kwa Sh187.8 milioni.
Alisema
katika kipindi hicho, wizara 17, balozi mbili na sekretarieti za mikoa
11 zilitumia zaidi ya Sh11.3 bilioni bila kuwapo vielelezo vyovyote,
hivyo kusababisha ashindwe kujua uhalali wa malipo hayo.
0 comments:
Post a Comment