Polisi
mkoani Mwanza imebaini mtandao unaohusika na ujambazi wa kuvamia,
kupora, kujeruhi na kuua wafanyabiashara wa maduka ya fedha.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tayari wamewatia mbaroni
watu watatu wanaodaiwa kuhusika na mtandao huo wakiwa na bunduki aina
ya SMG ikiwa na magazine nne na risasi 144.
Pia,
watuhumiwa hao walikutwa na kofia moja ya kuficha uso, hijabu mbili,
jaketi moja pamoja na mabegi mawili wanayotunzia silaha zilizokuwa
zimefichwa kwenye nyumba wanayoishi.
“Polisi
bado inaendelea kumsaka kinara wa mtandao huu (jina linahifadhiwa),
ambaye alifanikiwa kukwepa mtego wa polisi, tunawaomba raia wema kutoa
taarifa zitakazofanikisha kumtia mbaroni,” alisema SACP Msangi.
Alisema bunduki iliyokamatwa inaaminika kutumika katika matukio zaidi ya sita ya uporaji katika maduka ya fedha.
Hivi
karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga alisema vyombo vya
dola tayari vimebaini mitandao saba ya uhalifu mkoani Mwanza.
Kitwanga
ambaye pia ni mbunge wa Misungwi aliwaeleza wapigakura wake kuwa tayari
mitandao miwili kati ya hiyo saba ilikuwa imeangamizwa, huku jitihada
za kuangamiza iliyosalia zikiendelea.
0 comments:
Post a Comment