Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha
miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh4.5 milioni, mfanyabiashara
Huifang Ma baada ya kupatikana na hatia ya kuuza bidhaa na kushindwa
kutoa risiti kwa kutumia mashine ya kieletroniki.
Ma
ambaye ni raia wa China na mkazi wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la
Kariakoo, alihukumiwa kifungo hicho baada ya kukiri mashtaka mawili
yaliyokuwa yakimkabili likiwamo la kushindwa kujisajili kulipa kodi ya
ongezeko la thamani (Vat).
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said
Mkasiwa alisema kwa kuwa mshtakiwa alikiri mashtaka yanayomkabili,
anatakiwa kulipa faini au kwenda jela miaka mitatu. Hata hivyo, Ma
alilipa faini na kuachiwa huru.
Katika
hati ya mashtaka, ilidaiwa kuwa Machi 23, mwaka huu eneo la Karikaoo,
mshtakiwa alishindwa kutoa risiti za kieletroniki kwa mteja wake.
Ilidaiwa
kuwa siku hiyo mshtakiwa ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya HM Textile Co
Ltd iliyopo Mtaa wa Agrey, Kariakoo, alishindwa kutumia mashine za EFDs
kwa ajili ya kutoa risiti kwa wateja walionunua bidhaa dukani kwake.
Kosa la pili, mshtakiwa alishindwa kujisajili kama mlipa kodi wakati akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
0 comments:
Post a Comment