Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake, Siwema Edson.
Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki
‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa yupo kwenye harakati za kumsaidia mzazi
mwenzake, Siwema Edson (27) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita
alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kujipatia mali kwa
njia ya vitisho kutoka kwa kigogo mmoja serikalini aliyetajwa kwa jina
moja la Deo.
Katika msala huo, Siwema alidaiwa kutoa
vitisho kwa mlalamikaji akimtaka kumnunulia gari aina ya Honda CVR lenye
namba za usajili T103 DDU lakini pamoja na kutimiziwa matakwa yake
hayo, aliendelea kumtumia vitisho, akimtaka amtumie kiasi kikubwa cha
fedha za mtaji, ndipo mlalamikaji akatoa taarifa polisi kisha mrembo
huyo, akakamatwa ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita alitupwa jela.
Akipiga stori na gazeti hili mara baada
ya hukumu kutolewa mwishoni mwa wiki iliyopita Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza, Nay alisema tayari ameshatafuta mawakili wawili kwa ajili ya
kukata rufaa ili kama itawezekana mama mtoto wake huyo arudi uraiani.
0 comments:
Post a Comment