Mchungaji wa Kanisa la AGCT, Mbagala,
Samuel Mihogu amewataka watumishi wengine wa Mungu nchini hususan wa
jijini Dar kufanya mpango kwa kuchagua siku moja ili kukesha kwa maombi
ya kumlilia Mungu azidi kumlinda Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’,
Wikienda lina maneno yake.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa
wiki iliyopita jijini Dar, Mchungaji Mihogu alisema kuwa, kwa mwendo wa
Magufuli kikazi anaamini atazalisha maadui, hivyo watumishi wa Mungu
wanatakiwa kumwomba Mungu ashushe ulinzi wake juu ya rais ili wabaya
wake washindwe kwa kuanzia.
“Magufuli anafanya kazi kubwa sana na
nzito. Kutetea kwake wanyonge kwa kuwatumbua vigogo wanaokula pesa za
umma lazima kuna watu hawatapenda, kwa hiyo mimi nawaomba wachungaji
wengine tupange namna ya kutafuta siku moja tu ya kukesha Uwanja wa
Taifa au Leaders (Dar) kwa maombi ili kumlilia Mungu amshushie ulinzi.
“Najua serikali inampa ulinzi wa kutosha
lakini maandiko yanasema mlinzi wa kweli ni Mungu. Kwa hiyo pamoja na
ulinzi wa serikali, lakini Mungu lazima ahusike,” alisema mchungaji
huyo.
Akaendelea: “Kuhusu kulindwa hata
Magufuli mwenyewe analijua ndiyo maana katika hotuba zake zote anawaomba
Watanzania wamwombee kwa vile kazi anayoifanya ni ngumu.
0 comments:
Post a Comment