Msanii wa bongo fleva aliyekuwa akitamba na kibao cha 'My'
Ally Nipishe aliswekwa ndani kwa miezi mitatu akikabiliwa na tuhuma ya
kumiliki mali ya wizi kitu ambacho kilimpelekea kupotea katika game.
Akizungumza na Enewz Ally alikiri kukumbwa na shitaka hilo
na kudai kuwa aliuziwa gari hiyo na mwanamke wake ambaye pia alikimbia
baada ya sekeseke la polisi kuibuka.
“Ni
msichana ambaye nilikuwa na uhusiano naye na alikuwa akinisaidia
kimaisha kitu ambacho sikutegemea kama angekuja kunifanyia tukio kama
hili hata siku moja kwasababu nilikuwa namuamini sana ”, alisema Ally.
Aidha
Ally alisema kuwa tangu tukio hilo litokee wamemtafuta msichana huyo
bila mafanikio ikambidi kutumia gharama nyingi zaidi kwaajili ya kulipa
fidia kwa wenye mali ili kuimaliza kesi hiyo kuliko alivyowahi kusaidiwa
na msichana huyo.
0 comments:
Post a Comment