Mahakama ya Juu nchini Colombia imehalalisha rasmi ndoa za wapenzi wa jinsia moja nchini humo.
Hatua hiyo inaifanya Colombia kuwa nchi ya nne ya Amerika Kusini kuhalalisha ndoa hizo.
Wapenzi
wa jinsia moja nchini Colombia awali tayari walikuwa wameruhusiwa
kuungana na kuishi pamoja, na walipata manufaa mengi yanayohusiana na
ndoa ikiwa ni pamoja na urithi, malipo ya uzeeni na marupurupu ya afya.
Lakini hawakuwa wameruhusiwa kufunga ndoa rasmi jambo ambalo sasa limefanyika.
Uamuzi
huo ulitarajiwa kwa kiasi kikubwa baada ya uamuzi wa mahakama mapema
mwaka huu wa kukataa pendekezo la kuwataka wathibitishaji wa mahakama
kutosajili miungano ya wapenzi wa jinsia moja kama ndoa.
0 comments:
Post a Comment