CHAMA cha ACT-Wazalendo kimekuwa na mawasiliano na Dk. Wilbrod Peter Slaa, mwanasiasa nguli wa upinzani nchini, kuhusu uwezekano wa yeye kushiriki katika kampeni za Chama chetu kwa lengo la kuendeleza vita dhidi ya ufisadi nchini.
Tunamshukuru
sana Dk. Slaa kwa imani aliyo nayo juu ya chama chetu na uamuzi wake wa
kuikabidhi rasmi ACT-Wazalendo, mikoba yake ya vita dhidi ya ufisadi
nchini.
Dk.
Slaa anaamini kwamba chama chetu cha ACT-Wazalendo ndicho chama pekee
chenye uhalali na uwezo wa kupambana na ufisadi baada ya chama chake cha
zamani kuitelekeza vita hiyo. Dk. Slaa alikuwa ashiriki kikamilifu
katika kampeni za uchaguzi zinazoendelea kupitia jukwaa la
ACT-Wazalendo.
Alikuwa
aanze na Mkutano wa hadhara Mjini Iringa siku ya Jumatano tarehe 7
Oktoba 2015, na baadaye angeendelea na mikutano mingine katika majimbo
mbalimbali na kuhitimisha kampeni hizo katika Viwanja vya Mwembeyanga
Jijini Dar es Salaam, ambao ndio uwanja ambapo vita dhidi ya ufisadi
ilitangazwa rasmi mnamo tarehe 15 Septemba 2007.
Baada
ya tathmini ya kina chama cha ACT-Wazalendo kimejiridhisha kwamba hali
ya usalama wa Dkt Slaa ni ndogo sana kwa sasa kutokana na vitisho
mbalimbali anavyovipata.
Kutokana na hali hiyo ya vitisho dhidi ya usalama wake, chama chetu kimejiridhisha kuwa hakina uwezo wa kumhakikishia Dk. Slaa usalama wake atakapokuwa majukwaani.
Kutokana na hali hiyo ya vitisho dhidi ya usalama wake, chama chetu kimejiridhisha kuwa hakina uwezo wa kumhakikishia Dk. Slaa usalama wake atakapokuwa majukwaani.
Kwa
kuzingatia maelezo ya hapo juu, chama chetu kimefuta mikutano yote
ambayo Dk. Slaa alikuwa aifanye kupitia jukwaa la ACT-Wazalendo.
Chama kitaendelea kutambua mchango wake katika harakati za kukuza demokrasia na hasa bidii yake ya kujitoa katika kupambana na ufisadi nchini.
Tunamuahidi kwamba chama chetu kitaendeleza vita hii kwa bidii kubwa na juhudi zake kamwe hazitapotea.

Tunamtakia Dk. Slaa na familia yake maisha mema.
Samson Mwigamba
KATIBU MKUU
Jumatatu Oktoba 5, 2015.
0 comments:
Post a Comment