Tuesday, July 21, 2015

Video: Watangazaji wa NTV wampa Ray C ujumbe kuwa Aendelee tu kuota kwasababu haitakuja itokee awe na mahusiano na Rais wao


Kutoka kutangaza kutafuta mume Instagram hadi kukiri kumpenda Uhuru Kenyatta, Ray C anaendelea kutengeneza vichwa vya habari Afrika Mashariki.

Weekend hii muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila, aliamua kufunguka hisia zake juu ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Lemme tell u a lil secret about Uhuru!!!!I love this guy to death!I have had a crush on him for soooooo long!!!huwa namuota sana sana!!!!I love everything about him!His Attitude, His accent!Total Package,” aliandika Ray C.

Ujumbe huo umepokelewa kama moja ya vituko vilivyotokea hivi karibuni hasa ukizingatia kuwa Uhuru ni mume wa mtu. Kituo cha runinga cha NTV kiliipa nafasi habari hiyo kwenye taarifa yake ya habari ya saa tatu usiku:
Watangazaji hao wamesema Ray C aendelee kuota coz haitakuja itokee.


 
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger