Kijana mmoja huko Dallas amejiua bahati mbaya kwa kujipiga risasi wakati alipokuwa anasherehekea birthday yake ya kufikisha miaka 21 jumamosi iliyopita.
Polisi wa eneo hilo wamesema kuwa Joseph Perez alikua anasherehekea B'day yake alipochukua bastola na kuanza kupiga kwenye party yake kama ishara ya kusherehekea siku hiyo. Familia yake walimnyang'anya bastola hiyo,lakini baadae kijana huyo alifanikiwa kuichukua tena na kwa bahati mbaya alijipiga mwenyewe risasi.
Joseph alikimbizwa kwenye hospitali ya karibu katika eneo hilo ambapo baadae alifariki dunia.
Msemaji wa Polisi katika eneo hilo Melinda Gutierrez alisema kwamba inaaminika kuwa Pombe ndio ilikua chanzo au sababu ya kijana huyo kuanza kupiga risasi ovyo.
0 comments:
Post a Comment