Bridewell lilikuwa Gereza ndani ya Liverpool Uingereza ambalo lilijengwa tangu miaka ya 1550 hivi, liliwahi kubadilishwa matumizi yake kwa mara kadhaa lakini hii ya sasa hivi ni story tofauti yani.
Pata picha mahali kama Gereza la Segerea, Keko au Ukonga ambamo leo hii wanahifadhiwa watu ambao wanatumikia vifungo, utajisikiaje siku moja kuingia kulala ndani ya Gereza mojawapo ikitokea miaka hata kumi baadae Gereza mojawapo linageuzwa Hoteli ya Kifahari kabisa !!

Bridewell Prison ilikuwa zamani mtu wangu, watu wameamua pasibaki hivihivi, imetengezwa bonge la Hoteli na kuna vitu vichache ukiviona ndio utashtuka kwamba hapo palikuwa Gereza…
Mwonekano wa Koridoni
Karibu sana aisee, hapa ndio chumbani tayari !!
Chumbani kumependeza kiukweli.
Hapo wakati likiwa Gereza bado.
Wataalam wakiendelea na kubadili mambo ya huo mjengo.
Mwonekano wa korido.
Hapo ni katikati ya Hoteli, ambapo kwa zamani ungekuta wafungwa wakipiga zao story mchana au jioni.
Mwonekano wa mlango wa Gereza hapo zamani.
Mwonekano wa nje wakati mambo yakiendelea kubadilishwa.
Baada ya kuwa Hotel kwa sasa pataitwa Stay Central The Bridewell, katikati ya Liverpool Uingereza..
Hizi ni pichaz nyingine mtu wangu.
Jamaa anaekatisha hapo ndio msimamizi wa hii biashara mpya ya Hoteli ambayo lilikuwa Gereza.
Karibu mtu wa nguvu, hata usiogope mlango.. Sio Gereza tena ni Hoteli.
Ndani kila kitu ni safi, mpaka Gym ipo yani..
Hii picha ilipigwa mwaka 1994, Afande yuko attention kabisa na Sare yake ya kazi.
Kwenye moja ya kuta za Hoteli hiyo kulikutwa na haya maandishi, ‘Siku moja utakuwa huru’
Hiki kilikuwa chumba cha kufanyia Mahojiano watuhumiwa.
Unaweza ukaona pia kinachosimuliwa kwenye hii Video kuhusu Gereza lililogeuzwa Hoteli Uingereza.
0 comments:
Post a Comment