MUME wa mwanamke anayedaiwa kumkamata ugoni Askofu Dk Alex Malasusa
wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki
na Pwani, (DMP) anatafuta watoto waliotoroshwa kwa maelekezo ya Malasusa
na Jeshi la Polisi.
Akizungumza na MwanaHALISI online baada ya
kuachiwa huru kutoka polisi kwa tuhuma za kushambulia, amesema watoto
wake walichukuliwa na raia mmoja mjerumani aliyeolewa na mtanzania,
anaitwa Caroline Shedafa.
Caroline Shedafa ametuhumiwa kuwa ametumia mwanya wa malalamiko ya
Mwakilima na Malasusa kwa sababu ya urafiki alifanikiwa kuwatorosha
watoto hao na kwamba ana mpango wa kuwasafirisha kwenda nje ya nchi
wakati wowote.
MwanaHALISI limemtafuta Shedafa kwa tuhuma hizo, alipokea simu na
baada ya kuambiwa kuwa anaongea na MwanaHALISI alikata simu na kukataa
kuongea suala hili na mwandishi.
Malasusa anadaiwa kuwa anadaiwa kushirikiana na mfanyakazi wa
hospitali ya Muhimbili anayeitwa Julieti, aliyewaambia ndugu wa mume
anayenyang’anywa mke wake na malasusa kuwa atakiona.
“Huyu kaka anajidai mjuaji, hapati kitu, utaratibu uko tayari wa
kuwasafirisha watoto kwenda nje ya nchi na hatawaona tena, ataishia
kuwasikia tu, mimi ni mtu wa Karibu na Askofu Malasusa ndo nawaambia”.
Alinukuliwa dada huyo akiongea kwa ujasiri.
Hadi sasa watoto wanaotafutwa na baba yao ambao Jeshi la Polisi
linadaiwa kushirikiana na Malasusa licha ya taarifa zao kufika polisi
kituo cha Wazo na kutochukuliwa hatua ni Sijenuni, Sephania, na Simon
wote wanadaiwa kuwa watoto wa Venance Mwakilima.
Taarifa za leo usiku zilizofikiwa MwanaHALISI online zinadai kuwa
baadhi ya Maaskofu Jijini Dar es Salaam wameamua kujitokea kulinda
heshima ya uaskofu baada ya kudhalilishwa na Malasusa.
Maaskofu ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa kuwa si wasemaji wa vikao halali wamesema “hili suala tunalichukua.
Malasusa ana tuhuma nzito nchini, na baada ya gazeti kuandika watu
wamejitolea kujieleza tunaomba muda kesho (Jumanne) tutaliongelea
hadharani baada ya kukutana na mume wa me.
Aidha Malasusa hakupatikana kwenye simu zake wala kujibu ujumbe wa
simu aliotumiwa tangu juzi wakati gazeti la MwanaHALISI likiendelea
kufuatilia sakata hili.
Taarifa ambazo mwandishi anazo zinadai viongozi wakubwa wa serikali
wanaingilia suala hili, zinafuatiliwa na zitaandikwa kwenye gazeti la
MSETO…
CREDIT: MwanaHALISI
0 comments:
Post a Comment