Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ na msanii wa Bongo Fleva, Ally Salumu ‘Ally Nipishe’, wakijivinjali.
Mwigizaji asiyeishiwa habari kwenye ulimwengu wa sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ ambaye hivi karibuni alitaka kumzawadia gari msanii wa Bongo Fleva, Ally Salumu ‘Ally Nipishe’, wawili hao wamebambwa laivu waikioneshana mahaba niue.
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na shushushu wetu ilijiri wikiendi iliyopita kwenye hoteli inayofahamika kwa jina la Yuro iliyopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar, majira ya usiku.
Kwa mujibu wa mtoa ‘ubuyu’ wetu, awali, wawili hao walishuhudiwa wakiingia hotelini hapo wakiwa wameongozana kama kumbikumbi huku wameshikana mikono.
Shuhuda wetu alidai kwamba, baada ya kukaribishwa ukimbini walihudumiwa vinywaji ambapo Bozi alionekana akitoa fedha na kumlipa mhudumu huku akimhudumia Ally Nipishe kwa kummiminia kinywaji na kumnywesha kisha wakaangua vicheko na kubadilishana vinywaji.
Wakati hayo yakiendelea, baadhi ya wahudumu walionekana kuwachungulia kwenye mlango wa vioo kwa kutoamini kilichokuwa kinaendelea kwani walifika mbali zaidi na kuanza ‘kudendeka’ mithili ya makinda wa njiwa kisha kusepa na kutokomea kusikojulikana.
Mwanahabari wetu alipomvutia waya Bozi na kumuuliza kulikoni kufikia hatua hiyo alidai kuwa Ally Nipishe ni mwanaume aliyekuwa akimvutia kwa kipindi kirefu hivyo azma yake imetimia.
Kwa upande wa Ally Nipishe, alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema ameamua kuwa karibu na Bozi ili kumfariji bila kufafanua kivipi.
0 comments:
Post a Comment