SIASA
katika ubora wake! Nyota wa filamu nchini, Jacqueline Walper Massawe
‘Wolper’ amemchana staa mwenzake, Chuchu Hans kufuatia kutofautiana
kiitikadi kisiasa kati ya chama tawala (CCM) na Ukawa.
Awali,
Chuchu Hans alitangaza kuhamia Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) na
kushiriki kikamilifu kwenye uzinduzi wa kampeni zao uliofanyika katika
Viwanja vya Jangwani, Dar wiki iliyopita.
Lakini
ghafla, Chuchu alionekana akiwa amevaa sare za Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na kutangaza kwamba ameamua kurudi nyumbani, kitendo
kilichoonekana kumkera mno Wolper, ambaye amejipambanua kuwa ni mfuasi
namba moja wa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
“Sijui
huu uzalendo wa Tanzania utakuja lini, yaani wewe juzi tuwe wote na
sare uvae, leo umetusaliti kisa vijisenti sasa aliyekwambia Ukawa
tunapewa hela ukaja na mbwembwe zote nani? Sikuwa na lengo la kukuweka
hapa ila nataka niseme kitu kimoja, jamani hamna kitu kibaya kama
unafiki, tamaa na njaa, hii ni nchi yetu sasa tukihongwa wote ili tuwe
chama kimoja ukombozi utakuwa wapi,” ilisomeka sehemu ya waraka ambao
msanii huyo aliuweka katika mtandao wake wa Instagram.
Gazeti
hili lilimtafuta muigizaji huyo ambaye ni mpenzi wa Vincent Kigosi
‘Ray’ na alipotakiwa kuzungumzia jambo hilo, alifunguka:
“Sikutaka
kujibu, lakini nimwambie Wolper ingawa mimi nimewahi kuzaa, lakini yeye
ni dada yangu, kanizidi umri, kwenye siasa kila mtu ana haki ya kupenda
kule anakotaka mwenyewe. Ni kweli nilienda Ukawa, lakini baadaye
nikagundua hawana ‘ishu’ nimerudi zangu CCM.”
0 comments:
Post a Comment