Shehena kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini imenaswa katika bandari ya Zanzibar huku ikishuhudiwa na mawaziri wa serikali zote mbili wakiongozwa na waziri wa mali asili na utalii Mhe Khamis Kagasheki.
Shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea Philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na magunia mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa kusafirishwa kwenda Philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka husika za bandarini.
Wakiongea na wandishi wa habari katika bandari ya Zanzibar waziri wa nchi afisi ya rais utawala bora na idara maalum Mhe Haji Omar Kheri amesema hii ni janga kubwa la nchi na serikali kamwe haitokubali kuona wahusika wanaanchiwa na kuahidi sheria kufanya kazi yake ,kwa upande wake waziri Kagasheki ambaye aliwisili Zanzibar asubuhii kushuhudia shehena hiyo amesema ni lazima mtandao utokomezwe kwani utamaliza tembo wa nchii hii na kuipoteza rasilimali ya nchi.
0 comments:
Post a Comment