Wednesday, November 6, 2013

MSIBA: BAHATI BUKUKU AFIWA NA BABA YAKE MDOGO....


Bahati Bukuku.
MSIBA mkubwa umeikumba familia ya msanii wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku aliyefiwa na baba yake mdogo, Lwagha Amen Bukuku. Marehemu Lwagha amefariki jana asubuhi katika Hospitali ya Kardinali Ukonga jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Msiba upo nyumbani kwa Bahati Bukuku eneo la Tabata Kisukulu, Dar. Marehemu atazikwa Alhamisi, Novemba 7, 2013 katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.
GUMZO LA JIJI LINAMPA POLE BAHATI BUKUKU PAMOJA NA FAMILIA NZIMA YA MZEE BUKUKU KWA MSIBA HUU. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger