Tuesday, October 15, 2013

RAIS KIKWETE APENDEKEZA KUWA NYERERE DAY IWE SIKU ALIYOZALIWA NA SIYO SIKU ALIYOFARIKI DUNIA....

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amependekeza kuwa siku ya ‘Nyerere day’ inayoadhimishwa October 14 kila mwaka, iadhimishwe siku aliyozaliwa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
Rais kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wananchi mjini Iringa katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru, iliyoambatana na kumbukumbu ya baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.
 
Amesema anapendekeza siku hiyo iwe siku ya kuzaliwa ili watu washerehekee kwa furaha, wakikumbuka hotuba za Mwalimu.
 
Endapo mapendekezo ya rais yataungwa mkono, Nyerere day itakuwa  April 13, kwa kuwa mwalimu alizaliwa siku hiyo mwaka 1922.

Una  mtazamo  gani  juu  ya  pendekezo  hili?

-timesfm
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger