Tuesday, October 15, 2013

"TUKUTANE DAR LIVE J'5"...OMMY DIMPOZ

Omar Faraji Nyembo 'Ommy Dimpoz'.

KUONYESHA jinsi gani alivyojipanga kuporomosha burudani ya kufa mtu katika Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, msanii mahiri wa Bongo Fleva, Omar Faraji Nyembo 'Ommy Dimpoz' amewaambia mashabiki wake wote wakutane Dar Live siku ya Jumatano.
Mkali huyo aliyekuwa nchini Marekani atapiga shoo Dar Live Jumatano ambayo ni Sikukuu ya Eid sambamba na Mwamba wa Kaskazini, Joh Makini. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Dimpoz amewataka mashabiki wake kutokosa shoo hiyo maana itakuwa ya aina yake. Ameeleza kuwa yeye pamoja na timu yake ya Poz kwa Poz watakuwa ndani ya nyumba kuwapa raha mashabiki. Katika sikukuu hiyo, Bendi ya Twanga Pepeta nayo itatoa burudani sambamba na Profesa Calabash atakayewapa burudani watoto.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger