Ndugu watanzania wenzangu, Inasikitisha sana kuwaona ombaomba wengi katika maeneo mengi ya dodoma na eneo la Ubungo mkoani Dar es salaam na maeneo mengine ya mikoani wakiwa katika maeneo hayo kila siku. ..
Pamoja na kuwasaidia fedha kidogo msaada huo hautoshi kuwaondoa pale walipo kutokana na hali zao za kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi za kutumia nguvu.
Wakati serikali yetu ikipitisha bajeti zenye kutumia fedha nyingi kwa kulipana posho na mishahara minono kwa watumishi wa ngazi za juu hasa wabunge na mawaziri inatakiwa pia kuwakumbuka walemavu wale wasio na msaada wowote wa kuwafanya waishi kama watanzania wegine kwa kuwaanzishia vituo maalumu ambapo watapata huduma na kutunzwa ..
Naomba ndugu wananchi na wabunge tuishinikize serikali ili iweze kulifanyia kazi swala hili kwani hawakupenda kukaa chini na kunyeshewa na mvua wakiomba msaada.
0 comments:
Post a Comment