Saturday, March 30, 2013

JAMES MBATIA WA NCCR- MAGEUZI APONGEZWA KWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU ZOEZI LA UOKOAJI WA GHOROFA LILILOPOROMOKA JANA


Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi mh. James Mbatia ameonyesha mfano wa kuigwa katika kusaidia shughuli ya uokoaji wa waathirika wa jengo lililoanguka jijini Dar es Salaam tarehe 29.32013. Hayo yameelezwa na walioshuhudia jinsi kiongozi huyo wa upinzani alivyokuwa hodari katika kutumia ujuzi wake Kuokoa watu walio nasa katika Ghorofa Hilo

Tofauti na Viongozi Wengine wengi wao walichokifanya ni kwenda kwenye mitandao ya kijamii kulifanyia kejeli janga hili kubwa kwa taifa na Kujitafutia Umaarufu kupitia Facebook and Twiiter..Badala ya kusaidia uokoaji.


Kamera za waandishi wa habari zilifanikiwa kupata picha kadhaa za jinsi mh. Mbatia alivyoonyesha umuhimu wa kuweka siasa pembeni katika majanga na kutoa kipaumbele kwenye kuisaidia jamii kuwa salama kwanza.

Hongera mh. Mbatia.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger