KUELEKEA kutimiza mwaka mmoja kaburini, marehemu Steven Kanumba anatarajiwa kuibua simanzi upya kupitia filamu yake ya Power of Love itakayotoka Aprili 12, mwaka huu.
Akipiga stori na Stori 3, mdogo wa marehemu, Seth Bosco alisema filamu hiyo itasambazwa nchi nzima na Kampuni ya Steps Entertainment hivyo mashabiki watapata kuona vibweka vya marehemu kupitia filamu hiyo ambayo aliirekodi siku chache kabla hajafariki, Aprili 7, 2012.
“Ni bonge filamu kusema kweli, najua itawahuzunisha wengi lakini hakuna jinsi lazima itoke na watu waishuhudie,” alisema Seth.
Monday, March 11, 2013
FILAMU MPYA IITWAYO 'POWER OF LOVE' YATARAJIWA KUIBUA MAJONZI MAPYA.....!!
Weka Maoni yako Hapa
0 comments:
Post a Comment