Thursday, February 28, 2013

NORA ANASWA NA BWANA WA NISHA

STAA mkongwe wa filamu Bongo, Nuru Nassor ‘Nora’ amenaswa na mpenzi wa zamani wa mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’ anayefahamika kwa jina moja la Geofrey.
Salma Jabu ‘Nisha’.
Sosi makini aliyeomba hifadhi ya jina lake alimtonya paparazi wetu kuwa wawili hao ni wapenzi na wamekuwa wakionekana viwanja mbalimbali vya starehe, paparazi wetu aliwapigia misele na kufanikiwa kuwanasa wakiwa kwenye pozi za kimahaba katika Ukumbi wa Meeda, Sinza Dar Jumamosi iliyopita.
Walipoulizwa kama
ni wapenzi, Nora alikana na kusema wanashirikiana kuandaa kazi za filamu.
“Huyu (Geofrey) tunafanya naye kazi mbalimbali za filamu, hapa tumekuja kutembea mara moja kwani kuna ubaya?,” alihoji Nora.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger