Wednesday, December 19, 2012

SANDRA, NORA WANUSURIKA AJALI!!

Haruni San
WIMBI la ajali linazidi kuwatafuna mastaa wa Kibongo ambapo Jumamosi iliyopita, wasanii wa sinema za nyumbani, Salma Salmin ‘Sandra’, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Jasmini Nyaku walinusurika kufa baada ya gari walilokuwa wamepanda, kuacha njia na kupinduka hivyo kupata ajali mbaya
   
Gari  walilopata nalo ajali Salma Salmin ‘Sandra’, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Jasmini Nyaku.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wasanii hao walikuwa ndani ya gari aina ya Toyota Fun Cargo lenye namba za usajili T 402 CDU ndipo wakapatwa na msala huo maeneo ya ‘round about’ ya Mlimani City, Dar ambapo gari liliacha njia na kupinduka bila sababu ya msingi.
“Gari halikuwa spidi kiivyo lakini ghafla tukashangaa kuona linagonga ukingo wa barabara na kupinduka ndipo tulipoanza kuwapa msaada na kuwapeleka hospitali,” kilisema chanzo hicho.
Salma Salmin ‘Sandra’.
Nora alipopatikana alifunguka:
“Ilikuwa ghafla tu, tulikuwa mimi, Nyaku, Sandra na mumewe ndani ya gari. Dereva alikuwa Jasmini tukashangaa gari linaacha njia na kupinduka bila sababu yoyote.
“Nimepata majeraha madogomadogo mkononi, Sandra ndiyo aliumia zaidi kichwani, hivyo tulilazimika kumpeleka Hspitali Kwamama Ngoma, Mwenge kisha tukaambiwa tumhamishie Muhimbili alikolazwa hadi sasa hivi.”
Nuru Nassoro ‘Nora’.




Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger