MSHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dustan ‘Jack Maisha Plus’ amenusurika kupigwa risasi na mtu ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu juzikati katika Fukwe za Coco, jijini Dar ambapo Jack alikwenda kupumzika ndipo alipotokea mwanaume mmoja na kumtongoza, alipokataa ndiyo akataka kumpiga risasi.
“Ilikuwa balaa, nilimuomba msamaha huyo mwanaume japokuwa sikumkosea, aliponielewa nilirudi nyumbani muda huohuo kwa sababu nilipata mshtuko mkubwa,” alisema Jack.
0 comments:
Post a Comment