Na Gladness Mallya
MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Filamu na Muziki wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaonya wasanii wa kike wanaotoka katika filamu na kutaka kuingia kwenye muziki bila ya kujipanga.
Akichonga na Tollywood Newz, Shilole alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii wa kike wanaotoka katika filamu na kutaka kuingia kwenye muziki baada ya kumuona yeye anavyosumbua.
“Wengi wanataka kushindana na mimi lakini nawaambia kuwa hawataweza kufikia levo niliyonayo kwa kuwa nimejipanga kisawasawa,” alisema.
Mbali na hivyo, Shilole amewataka wasanii hao wa kike ambao wameshaanza kumtengenezea bifu kuwa hawatamuweza kwani yeye ni mpiganaji asiyebweteka.
MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Filamu na Muziki wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaonya wasanii wa kike wanaotoka katika filamu na kutaka kuingia kwenye muziki bila ya kujipanga.
Akichonga na Tollywood Newz, Shilole alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii wa kike wanaotoka katika filamu na kutaka kuingia kwenye muziki baada ya kumuona yeye anavyosumbua.
Mbali na hivyo, Shilole amewataka wasanii hao wa kike ambao wameshaanza kumtengenezea bifu kuwa hawatamuweza kwani yeye ni mpiganaji asiyebweteka.
0 comments:
Post a Comment