Friday, October 26, 2012

Miss TANZANIA Salha Israel anusurika kuibiwa GARI usiku!

WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi juzikati walivamia nyumbani kwa Miss Tanzania 2011, Salha Israel maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar na kufanya jaribio la wizi.Akizungumza na Ijumaa, Salha alisema tukio hilo lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku ambapo watu hao wasiofahamika waliruka ukuta na kutaka kufanya uhalifu lakini walishitukiwa kabla ya kutekeleza mpango huo.

“Sijui niseme ni wezi au majambazi ila ilikuwa saa 8 usiku, watu hao waliruka ukuta wakaingia ndani. Hutujui kama walitaka kuondoka na gari au kuiba vitu vilivyokuwemo ndani yake lakini walivunja kioo cha mbele.
“Kwa bahati tulisikia vurugu zao na kabla ya kuiba chochote, tuliwakurupusha na ndipo walipokimbia,”
alisema Salha.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger