Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza
katika mkutano wa wadau mawasiliano juu uzimwaji wa simu feki leo katika
ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wa mawasiliano wakimsikiliza mkuu wa mkoa leo jijini Dar es Salaam.
Watanzania wametakiwa kutumia simu zenye viwango na kuachana simu bandia ambazo hata kiafya si salama kwa matumizi ya binadamu.
Hayo
ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati
mkutano wa wadau wa mawasiliano kuelekea uzimaji wa simu leo usiku wa
kuamkia kesho, Makonda amesema TCRA imethubu kutoa huduma bora kwa
wananchi katika mawasiliano.
Amesema
TCRA imeweza kupambana tangu uzimaji wa analojia kuingia digitali
ambapo Tanzania imekuwa nchi ya mfano katika utekelezaji wa vitendo
katika masuala mawasiliano.
Makonda
amesema hata katika sheria ya mtandao baadhi ya watu walikuwa wanapinga
ili kuweza kuendelea kutukana katika mitandao ambapo TCRA imeweza
kufanikiwa kufanya hivyo.
Makonda amewataka wadau kuja na mawazo ya kuboresha huduma ya mawasiliano nchini katika ulinzi wa taifa.
0 comments:
Post a Comment