Mamlaka ya Misri imesema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka
katika bahari ya Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini
na sita yameweza kubainika yalipo.
Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali
hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza
kubaini maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha
ya kwanza ya masalio hayo.
Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani
wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo
iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris
kuelekea Cairo.
Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini
hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha
ndege hiyo.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment