Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema,
ingawa idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na uhakika wa maisha yao wala
kazi zenye tija na staha wapo katika nchi zinazoendelea, dunia katika
ujumla wake inapashwa kuonyesha utashi wa kisiasa na udhubutu wa
kuwekeza kupitia vijana.
Amesema,
mazingira ya mamilioni ya vijana kukaa bila shughuli ya aina yote
kunatoa mwanya kwa vijana hao kurubuniwa na kutumiwa na watu
wasiokuwa na nia njema na hivyo kutishia hali ya Amani, usalama na
ustawi wa mwanadamu na hatimaye kushindwa kufikia au kupata faida za
kidemografia na maendeleo endelevu.
Mhe.
Kikwete ameyasema hayo ( jumanne) hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa, wakati alipotoa mhadhara wa 13 wa kumbukumbu ya Rafael M.
Salas. Mhadhara huu ambao mada yake ilikuwa ni “ kuwekeza kwa vijana
ili kupata faida ya kidemografia na maendeleo endelevu” uliandaliwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu( UNFPA) ikiwa ni
sehemu ya mikutano ya mwaka ya Bodi za Mashirika na Mifuko iliyopo
chini ya Umoja wa Mataifa.
Miongoni
wa viongozi waliohudhuria na kushiriki mhadhara ni pamoja na
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson, na
Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin , Bi. Carmelita
R. Salas ambaye ni Mjane wa Bw. Rafael Salas aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa kwanza wa UNFPA, Mabalozi na wataalamu mbalimbali.
“Tafiti
na taarifa mbalimbali zikiwamo za Umoja wa Mataifa, zinaonyesha wazi
ongezeko la idadi kubwa ya vijana wanaokadiriwa kufikia 1.8 bilioni
idadi ambayo ni hazina na raslimali kubwa, lakini pamoja na uwingi wao,
wengi bado wanaishi katika hali ya umaskini uliokidhiri, na ukosefu wa
fursa mbalimbali ambazo zingewazesha kuishi maisha yenye staha”. akasema Kikwete.
Na
kuongeza kuwa, kati ya vijana hao 1.8 bilioni, 74 milioni hawana
ajira akiwaelezea kama vijana wanaosubiri treni kando ya reli, treni
ambayo haiji. Mazingira haya yanadhihirisha upotevu wa raslimali
kubwa ambayo imewekezwa kwa vijana hao na ambao wamepoteza matumaini.
Akafafanua
zaidi kwa kutoa takwimu mbalimbali zinazoonyesha tofauti ya faidia za
kidemografia kati ya mabara ya Ulaya, Asia, Amerika ya Latini na
Afrika ikiwa ni pamoja na utofauti wa matumizi ya raslimali watu kwa
nchi zile ambazo zimethubutu kuwekeza kwa vijana.
Rais
Mstaafu Kikwete katika mhadhara wake huo na ambao ulipokelewa vema
sana na wajumbe waliohudhuria, pia ametoa vielelezo vya kitakwimu
vinavyoainisha namna gan bara la Afrika lilivyo nyuma karibu
katika ikielemewa kila eneo kuanzia upatikanaji na utoaji wa huduma
za uzazi salama, idadi ya wakunga wenye elimu ya kutosha, upatikanaji
wa huduma za afya, elimu, maendeleo ya kijamii na yenye tija na
stahiki na kiwango cha matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango.
“Vijana
wakiwezeshwa, wakiaminiwa, wakipewa fursa na wakithubutishwa wanauwezo
mkubwa sana wa kuleta mabadiliko. Tunatakiwa kuwaamini, tunatakiwa
kuwashirikisha na kusizisikia sauti zao” amesema.
Na
kuongeza kuwa , mipango na sera zinazoandaliwa kwaajili yao vijana ni
vema zikawa shirikishi na kuzingatia mawazo, maoni na matakwa ya
vijana.
“Haya
na mengi mengi yakitekelezwa kwa kuzingatia mazingira ya kila nchi na
vipaumbele vyake, tunaweza kugema nguvu kazi hii kubwa kujiletea
maendeleo endelevu pasipo kumwacha yeyote nyuma” akasisitiza Rais Mstaafu.
Katika
hotuba yake hiyo iliyosheni takwimu na utafifi wa kisayasi, siyo tu
kwamba imeainisha hali halisi ya mazingira waliyomo vijana bali pia
imechochea majadiliano na takafuri ya kina.
Baadhi
ya mambo ambayo ameyatilia mkazo ni pamoja na umuhimu wa jamiii
kuzingatia uzazi salama na wa mpango na kuwa na idadi ndogo ya watoto
na ambayo wazazi wataweza kuimudu na elimu itakayokidhi mahitaji ya
soko la ajira lishe bora na uchumi imara na endelevu.
Akimkaribisha
Rais Mstaafu kuzungumza, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan
Elliason pamoja na mambo mengine alimwelezea Mhe. Kikwete kuwa ni
kiongozi mpenda amani na aliyemstari wa mbele katika kusimamia afya
ya mama na mtoto.
0 comments:
Post a Comment