SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar
es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la upatikanaji wa huduma
ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Maji wa Ruvu Juu,
jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo yote ya mji wa Kibaha mkoani
Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 72, kuanzia siku
ya Ijumaa 17/06/2016, Jumamosi 18/06/2016 na Jumapili 19/06/2016.
Akizungumzia
kukosekana Kwa huduma hiyo ya Maji, Kaimu Meneja Uhusiano wa DAWASCO,
Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza sababu ya kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu
Juu, ni kumruhusu Mkandarasi (WABAG) kuunganisha mtambo mpya wa Maji na
ule wa zamani, ambapo baada kukamilika kwa kazi hiyo, uzalishaji wa Maji
utaanza mara moja.
“Tuko kwenye hatua ya mwisho ya
kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani, kazi hii ikikamilika,
uzalishaji utapanda kutoka wastani wa lita Milioni 70 hadi kufikia lita
Milioni 106 kwa siku hivyo kuweza kutimiza lengo letu la kumtua mama
ndoo ya Maji kichwani” alisema Lyaro
Lyaro, ameeleza kuwa kuzimwa kwa mtambo huo, kutasababisha maeneo ya Mlandizi,
Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na
eneo lote la Tabata, Segerea hadi Kinyerezi kukosa huduma ya Maji.
Hivyo, ametoa
wito kwa wateja na wananchi wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia
kwa matumizi muhimu na lazima ili kukidhi mahitaji yao kwa kipindi
chote cha kukosekana kwa huduma hiyo.
0 comments:
Post a Comment