Yanga imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
kuafutia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United jioni ya leo Uwanja
wa Kambarage, Shinyanga.
Ushindi huo ulitokana na mabao mawili ya washambuliaji wa kimataifa
wa Zimbabwe, Donald Ngoma na Amissi Tambwe wa Burundi, unaifanya Yanga
ifikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 27.
Yanga sasa inaweza kutangaza ubingwa ndani ya mechi mbili zijazo kati ya tatu za mwisho, iwapo itaendeleza wimbi la ushindi.
Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, Yanga tayari walikuwa mbele kwa
mabao 2-0, yote yakifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe,
Donald Ngoma.
Ngoma alifunga bao la kwanza dakika ya pili kwa shuti kali, baada ya
kuupitia mpira kwenye himaya ya mabeki wa Stand, Nassor Masoud ‘Chollo’
na Assouman David.
Ngoma tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 45 kwa bao
zuri akimlamba chenga kipa wa Stand United, Frank Muwonge baaada ya
kutanguliziwa pasi nzuri na Mrundi, Amissi Tambwe.
Kipindi cha pili, Yanga ilikianza vizuri tena na kufanikuwa kupata
bao la tatu lililofungwa na Tambwe dakika ya 63 akimalizia kona ya winga
Simon Msuva.
Elias Maguri akaifungia bao la kufutia machozi Stand United dakika ya
82 baada ya kiungo wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kumchezea rafu
kiungo wa Stand, Suleiman Kassim ‘Selembe.’
Yanga waliendelea kulisakama lango la Stand, lakini bahati yao leo ilikuwa ni 3-1.
0 comments:
Post a Comment