Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Matemela
aliyefahamika kwa jina la HUSSEIN BAKARI (59) baada ya kukutwa na miche
25 ya Bangi akiwa amepanda kwenye bustani yake ya mbogamboga.
Mtuhumiwa
alikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.05.2016 majira
ya saa 16:00 jioni katika Kijiji cha Mayota, Kata ya Lugelele, Tarafa ya
Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.
Aidha katika
msako mwingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la WILSON PHILIP (19)
mwendesha Pikipiki/bodaboda, mkazi wa Msasani anashikiliwa na Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya akiwa na Bangi yenye uzito wa Gram 10.
Mtuhumiwa
alikamatwa na askari katika msako uliofanyika mnamo tarehe
01.05.2016 majira ya saa 17:05 jioni huko Mtaa wa msasani, Kata ya
Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Imesainiwa na:
(EMANUEL G. LUKULA – ACP)
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment