Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tologo iliyopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita wanajisaidia mlimani kutokana na ukosefu wa vyoo.
Pia, shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa madarasa na ofisi za walimu, jambo lililomlazimu Mwalimu Mkuu, Charles Mazara kutumia nyumba ya mwalimu kama darasa.
Pia, shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa madarasa na ofisi za walimu, jambo lililomlazimu Mwalimu Mkuu, Charles Mazara kutumia nyumba ya mwalimu kama darasa.
Akizungumza na gazeti hili, Mazara alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 ina wanafunzi 672 wa darasa la kwanza hadi la saba na kwamba na ina madarasa matatu, hivyo kuwa na upungufu wa madarasa 14.
“Tuna changamoto kubwa ya matundu ya choo na madarasa. Yalikuwapo matundu sita yalititia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha,” alisema.
Mazara alisema mwamko mdogo wa elimu kwa wazazi na walezi ni chanzo cha wanafunzi kukosa vyoo na madarasa kwa kuwa hawako tayari kuhudhuria vikao vya kujadili kukabiliana na changamoto hizo.
Mbali na changamoto hizo, shule hiyo pina inakabiliwa na upungufu wa madawati 280. Kwa sasa ina madawati 60 pekee.
Kaimu Mratibu wa Elimu wa kata hiyo, Sospeter Semi alisema watajitahidi kuhakikisha tatizo la matundu ya choo linamalizika hivi karibuni.
“Tumekubaliana kuanza ujenzi wa matundu ya choo, baadaye tuanze mkakati wa kujenga madarasa,” alisema Semi.
Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo, Abdallah Mchele aliahidi kuwakutanisha wazazi ili waweze kutatua tatizo hilo.
Alisema jukumu la kuhakikisha afya za wanafunzi wawapo shuleni liko mikononi mwa wazazi na walezi, hivyo watahakikisha wanalitekeleza haraka ipasavyo.
0 comments:
Post a Comment