Baada ya South Africa kusema kuwa Media
za Nyumbani zitaplay muziki wa nyumbani kwa asilimia 90, msanii toka
Label ya WCB Diamond Platnumz amefunga mawazo yake.
Akizungumza na Ayo TV staa huyo alisema…‘Wasanii
wanatakiwa kutengeneza nyimbo kali ili media mbalimbali ziweze kuacha
kucheza nyimbo za nje, kwa mfano zamani tulikuwa tukitoa baadhi ya video
zinakubalika lakini sio kama video za nchi jirani lakini tulivyoanza
kushoot video nzuri wenyewe wanaamini kuwa video za vijana wao ni kali’-
Diamond Platnumz
‘Tukumbuke
zamani watu walikuwa wanapenda sana movie za nchi za nje za kutoka East
Africa, Nigeria na nchi zingine lakini walivyoanza wakina marehemu
Kanumba, Ray kutengeneza movie soko lilikufa la watu wa nchi za nje
tulikuwa tunapenda movie za kitanzania kwahiyo nasema tuache kulalamika
tutengeneze kitu ambacho ni kizuri na kitapendwa zaidi kuliko kile cha
nchi jirani’- Diamond Platnumz
0 comments:
Post a Comment