Harmonize na Jacqueline Wolper ni couple mpya town. Kwa wengi
katika hatua za mwanzoni walidhani wawili hao si wapenzi bali
wanatafuta tu kiki.
Lakini kadri siku
zinavyoendelea kwenda, tumeshuhudia kuwa ni kweli wawili hao ni wapenzi
na wanaonekana kudatishana haswaa. Kuna sababu nyingi zilizofanya watu
wasiamini uwepo wa couple hiyo na kubwa zaidi likiwa ni miezi michache
iliyopita Wolper alichumbiwa na mwanaume mwingine na tukaamini kuwa sasa
mrembo huyo ameamua kuanzisha familia.
Hivyo baada ya kumuona akiwa na bwana mdogo Harmonize,
maswali yalikuwa mengi ya kuhusu kipi kilichotokea katika uchumba wake
na mwanaume huyo.
Sababu
ya pili ni utofauti wa umri kati ya wawili hao. Harmonize ni mdogo mno
kwa Wolper japo wanasema mapenzi hayaulizi kwanini na umri si kitu bali
ni namba tu.
Hata hivyo kwa showbiz, uhusiano huo utamfaidisha zaidi Harmonize
ambaye anaonekana kufuata nyayo za bosi wake kwa kuziteka headlines kwa
story za uhusiano na mastaa.
Wakati ambao kila mtu ameshathibitisha kuwa wawili hao ni
wapenzi, baadhi ya watu wanadhani kuwa mapenzi yao yamekuwa na chumvi
nyingi ndani ya muda mfupi na ni kama wanalazimisha watu waamini kuwa
wanapendana.
Katika wiki mbili hizi, post nyingi
za Wolper ni za picha yake akiwa na mpenzi wake huyo ambaye yeye amuita
Raj. “Pale mahaba yanapozidi paka macho yanaanza kufanana, u have my
heart Raj,” ameandika kwenye picha moja.
Harmonize bado ana aibu kiaina
kuanika penzi lao lakini amekuwa akitupia picha mbili tatu za Wolper
anayemuita pacha wake.
Lakini wawili hao wamekuwa
gumzo zaidi wiki baada ya kuhudhuria kwenye birthday ya mtoto wa Aunty
Ezekiel na Mose Iyobo, Cookie aliyetimiza umri wa mwaka mmoja. Wakiwa
mbele ya Diamond na wageni wengine waalikwa, hawakuonekana kutoshana
kwakuwa muda mwingi walikuwa wakishikana na kubadilisha mate bila aibu.
Video inayowaonesha ‘love birds’ hao wakibadilishana mate
hadharani imesambaa mtandaoni na kuzusha maswali mengi kuhusiana na
jinsi wanavyoupeleka uhusiano wao. Kwa wengi wanaona kama wana show off
zaidi na kwamba uhusiano wao umebeba picha ya kiki kuliko uhalisia wa
watu wawili wanaopendana.
Kwenye video hiyo
Diamond anaonekana kutojali kilichokuwa kikiendelea kulia kwake wakati
kijana wake Harmo alikuwa akishushiana mabusu na mafrench kiss ya
kumwaga na ex wa bosi wake.
“Mkwe leo mmejua kutuchafulia insta… yani kama sabuni ya unga uliyontolea watu MAPOVU,” ameandika Diamond kwenye post yake.
0 comments:
Post a Comment