Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo, inatarajia
kutoa uamuzi wa kupokea au kutopokea kiapo cha ushahidi katika kesi ya
kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Ukonga,
Jerry Silaa (CCM) dhidi ya mbunge Mwita Waitara (Chadema).
Kesi
hiyo namba 10 ya mwaka 2015 aliifungua Novemba, mwaka jana dhidi ya
mbunge huyo, msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ukonga na Mwanasheria Mkuu
wa Serikali (AG), akipinga ushindi wa mbunge huyo.
Wakili Mkuu
wa Serikali, Gabriel Malata aliiomba Mahakama kutopokea hati ya kiapo
hicho kilichowasilishwa na Silaa akiongozwa na wakili wake, Dk Masumbuko
Lamwai kutokana na kukosewa.
Wakili Malata akishirikiana na
Dk Onesmo Kyauke waliweka pingamizi hilo kwa kuwa kiapo hicho kimekiuka
matakwa ya sheria kwa kuwasilisha nakala halisi zote badala ya nakala
iliyotokana na nakala halisi.
Jana, Mahakama ilipanga kuanza kusikiliza kesi hiyo na Silaa alitarajiwa kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji Fatuma Masengi.
0 comments:
Post a Comment