Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi
Sakata
la kuhamishwa kwa wafanyabiashara wadogo katikati ya Jiji la Dar es
Salaam limeingia mdudu baada ya madiwani wa Ukawa kugomea uamuzi
uliotolewa na uongozi wa jiji hilo.
Uamuzi
huo uliotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi,
unadaiwa kutowashirikisha wadau hao na wafanyabiashara wenyewe.
Mwenyekiti
wa madiwani wa Ukawa, Manase Mjema amesema Mngurumi ametoa umuzi huo
bila pia kumshirikisha hata Meya wa Ilala, Charles Kuyeko.
Wamesema
masoko ya Kivule, Tabata Muslim, Ukonga na Kigogo Fresh ambayo
mkurugenzi huyo amesema yametengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao,
hayajaboreshewa miundombinu yake ikiwamo ujenzi wa vyoo na mabomba ya
maji.
Wamemtaka kusitisha mchakato huo mpaka watakapo jadiliana tena.
0 comments:
Post a Comment