Tuesday, May 10, 2016

Swissport yajenga bohari ya kisasa iliyogharimu shilingi bilioni 26 za kitanzania

Swissport Tanzania Plc, ambayo ni kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora za kupakia na kupakua mizigo na kuhudumia abiria duniani, imeboresha huduma zake baada ya kujenga bohari ya kwanza ya kisasa katika bara la Afrika iliyogharimu shilingi bilioni 26 za kitanzania.

Matarajio ya ukuaji wa huduma za usafirishaji kwa ndege yatakuwa ni ndoto kama hakuna huduma bora za kupakia na kupakua mizigo nchini,alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Swissport Bw Gaudence Temu wakati wa ziara ya waandishi wa habari walipotembea ofisi za Swissport zilizopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

Sekta ya usafiri wa anga ni nyeti, ambayo uwepo na ukuaji wake unategemea huduma zinazoaminika kama vile pamoja na mambo mengine utunzaji na usimamizi wa mizigo, bohari, utunzaji na usimamizi wa barua, utunzaji wa nyaraka zinazohusu mizigo iliyopakiwa au kupakuliwa.

Bw Temu alisema kwamba uzinduzi rasmi wa jengo hilo jipya la kuhudumia mizigo inayoingia na kutoka nchini litazinduliwa rasmi mwezi ujao baada ya ujenzi wake wote kukamilika rasmi.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger